Wednesday, June 27, 2012

BREAKING NEWS: PICHA ZA Dk. ULIMBOKA BAADA YA KUTEKWA NA KUPIGWA VIBAYA




PICHANI: Dkt. Ulimboka akiwa katika hali mbaya mara baada ya kuokotwa akiwa hajitambui.

Taarifa iliyonifikia (JamiiForum) hivi punde ni kuwa jemedari Dr. Ulimboka ametekwa majira ya saa sita usiku na watu watatu waliokuwa na silaha za moto na kumpeleka kusikojulikana! Inasemekana alipigiwa simu na jamaa mmoja aliyejitambulisha kwa jina moja la 'Abeid' ambaye tangu mwanzo amekuwa akiwasiliana naye na kujiita afisa wa serikali na kudai kuwa alitaka aonane naye face to face kwa ajili ya reconciliation.

Taarifa zimekwisha fikishwa polisi na sehemu zingine kwa ajili ya ufuatiliaji. (source chanzo cha kuaminika).

UPDATE:
Inaelekea waliomteka si watu wema kabisa, Dr. Ulimboka kaokotwa sehemu akiwa katika hali mbaya sana!

By Riwa:
Jamani this is is serious; Nimepigiwa simu sasa hivi na watu wa Legal and Human Rights Center wameniambia wametoka kumchukua Dr. Ulimboka kule Mabwepande amepigwa vibaya sana na ni emergency wanampeleka MOI sasa hivi.

Please tunaomba mtume habari hii kila mahali please!

Ni habari ya uhakika sana nimeomngea na Patience Mlowe wa Legal and Human Rights center.

Chanzo: Colleague ambaye yuko naye sasa!

JamiiForum

No comments:

Post a Comment