Tuesday, May 22, 2012

BREAKING NEWS............AJALI MBAYA YACHINJA WATATU IRINGA ASUBUHI HII









Ajali mbaya imetokea mjini Iringa asubuhi hii na kusababisha vifo vya watu watatu papo hapo huku abiria waliokuwemo katika fuso wakinusurika katika ajali hiyo .

Mashuhuda waliozungumza na mtandao wa http://www.francisgodwin.blogspot.com/ wamedai kuwa Taxi hiyo yenye namba za usajili T620 ANE ilikuwa ikitokea Ndiuka ikiwapeleka wafanyakazi wa barabara katika eneo la Tanangozi ambako ujenzi wa barabara kuu ya Iringa -Mbeya uinaendelea .

Hata hivyo kabla ya kufika katika eneo hilo la kituo cha Mafuta cha Eso dereva wa Taxi hiyo ambaye alikuwa akitaka kulipita gari jingine lililokuwa mbele yake alishindwa kulipita gari hilo baada ya kukutana uso kwa uso la Fuso yenye namba za usajili T897 AQS ambalo lilikuwa limeshehena magunia ya mpunga .

Hivyo kutokana na mwendo kasi ambao Fuso hilo lilikuwa likienda nao na mwendo kasi wa Taxi hiyo uwezekano wa kukwepana ulishindikana na hivyo kupelekea fuso hilo kuigonga Taxi hilo na kuipitia kwa juu na kupelekea vifo vya abiria wawili na dereva wa Taxi hiyo papo hapo .

Jitihada za kuzitoa maiti hizo zinaendelea hadi sasa japo eneo la tukio likiwa limetapakaa ubongo wa maiti hizo za ajali na wasamaria wema wakiendelea kufanya kazi hiyo ya kuzitoa maiti bila ya kutumia kinga yeyote na hivyo idadi kubwa ya wasamaria wema hao wameonekana wakiwa wametapakaa damu.

Na Francis Ngowi

No comments:

Post a Comment