Mwigizaji Maarufu wa filamu za Kibongo Elizabeth Michael ‘Lulu’ jana majira ya saa nne asubuhi amepandishwa kizimbani kwa mara ya pili katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam na kusomewa shitaka la kumuua Steven Kanumba. Baada ya kusomewa shitaka hilo na Mwendesha Mashitaka Mkuu wa Mahakama hiyo Elizabeth Kaganda mbele ya Hakimu Rita Tarimo hakutakiwa kujibu lolote. Mwendesha Mashitaka huyo alisema upelelezi wa kesi hiyo bado haujakamailika hivyo kesi hiyo iliahirishwa mpaka Mei 7 mwaka huu.
PICHA ZOTE NA RICHARD BUKOS/GPL
No comments:
Post a Comment