KATIKA hali inayoonekana si ya kawaida, beki wa pembeni wa Yanga, Stephano Mwasyika, amesema ataandika barua kwa mwamuzi, Israel Nkongo.
Mwasyika alimtandika Nkongo ngumi katika mechi ya Ligi Kuu Bara dhidi ya Azam FC Jumamosi iliyopita na kusababisha afungiwe kucheza soka kwa mwaka mmoja.
Akizungumza katika mahojiano maalum na Championi Ijumaa, Mwasyika alisema amechukua uamuzi wa kuandika barua kwa watu kadhaa akiwemo Nkongo.
“Ninajutia kosa langu, najua kuna mengi yametokea na mwisho nimegundua sikustahili kufanya vile. Kitu kibaya ilikuwa ni kushindwa kudhibiti hasira zangu, nimeamua kuandika barua kwa Nkongo nimuombe msamaha.
“Nitamwambia aniwie radhi kwa kuwa sikupanga kufanya vile, nilimdhalilisha. Lakini pia nitakiandikia chama cha waamuzi (Frat), ambao ndiyo wanamuongoza Nkongo. Nitafanya hivyo kwa TFF na klabu yangu.
“Nimeamua pia kuwaomba radhi wachezaji wenzangu kwa usumbufu wowote niliosababisha. Mwisho ninaomba mnifikishie kauli ya kuomba msamaha kwa mashabiki wa Yanga,” alisema Mwasyika, beki aliyechipukia kisoka akiwa Prisons ya Mbeya na kuongeza:
“Soka ndiyo kazi yangu, nisingependa kuingia kwenye matatizo yaliyotokea na wala sitaki kujitetea sana kwa kuwa yaliyotokea kila mmoja aliona. Naomba pia familia yangu inisamehe kwa hilo.”
GPL

No comments:
Post a Comment