Monday, March 19, 2012

KUDADEKI PATI YA BONGO MOVIE...


SHEREHE ya kutimiza mwaka mmoja tangu kuanzishwa kwa Klabu ya Bongo Movie iliyofanyika usiku wa kuamkia Machi 17, mwaka huu ilitia fora na kila mgeni aliyepata mwaliko alifarijika kwa namna yake.

Kabla ya kuanza rasmi kwa sherehe hiyo, mwenyekiti wa klabu hiyo, Jacob Steven ‘JB’ alianza kutambulisha viongozi wenzake na baadaye kukabidhi kipaza sauti kwa mshereheshaji Steven Mengele ‘Steve Nyerere’ kuongoza sherehe hiyo.

Baada ya kufanya hivyo, ukafuatia mpango mzima wa kukata keki, ambapo Steve Nyerere alimwalika jukwaani mtoto wa Rais wa Jamhuri ya Tanzania, Ridhiwan Kikwete kuendesha zoezi hilo.

LULU ASAHAU CHEO CHAKE
Kituko cha kwanza kilianza pale mwigizaji wa filamu, Elizabeth Michael ‘Lulu’ alipoambiwa ajitambulishe cheo chake na kushindwa kufanya hivyo.

“Mi’ mwenzenu kusema ukweli cheo changu sikifahamu, nimepandishwa tu hapa juu,” alisikika Lulu na kusababisha watu kuangua vicheko hadi pale Vincent Kigosi ‘Ray’ na JB walipomsaidia kumtajia cheo chake cha mjumbe wa bodi ya Bongo Movie.

WATU WAKIMBIA VINYWAJI NA CHAKULA
Jambo lingine ambalo lilikuwa la aina yake ni pale wageni waalikwa walipoondoka huku wakiwa wamesaza vinywaji na chakula.

“Hii sherehe ni kiboko, watu wamekula na kunywa hadi kusaza jinsi vyakula na vinywaji vilivyokuwa vingi,” alisema mmoja wa waalikwa.

WEMA AENDELEZA UPEDESHEE WAKE
Mwigizaji asiyeishiwa vituko, Wema Sepetu aliendeleza upedeshee wake jukwaani baada ya kwenda kuwatuza Steve Nyerere, Single Mtambalike na JB walipokuwa wakiimba wimbo wa ‘Pesa Position’ ulioimbwa na Lwambo Lwanzo Makiad.

Wema alimwaga fedha jukwaani kwa staili ya aina yake huku akiwaacha midomo wazi baadhi wa watu waliofika katika tukio hilo.

VAZI LA WOLPER LASISIMUA WATU
Vazi alilokuwa amevaa mwigizaji, Jacqueline Wolper liliwasisimua baadhi ya wanaume waliobahatika kuliona kwani upande wa mbele liliacha wazi sehemu kubwa ya mwili wake na kufanya matiti yake kuzibwa na sidiria tu.

Tukio la mwisho katika pati hiyo lilikuwa ni lile la kutoa tuzo za heshima kwa wasanii na wadau mbalimbali waliofanikisha maendeleo ya Bongo Movie.

Waliopata tuzo hizo ni Ridhiwan Kikwete, Mbunge wa Mvomero, Amos Makala, Mama Rolaa na wafanyabiashara mbalimbali ambao tuzo zao zilipokelewa na wawakilishi wao.

Kwa upande wa wasanii, Wolper, Steve Nyerere, Mainda, Ray, JB, Richie na wengine walipata tuzo kwa mchango wao kwa kundi hilo.


Na Waandishi wa GPL

No comments:

Post a Comment