Monday, March 26, 2012

KESI YA KAJALA MASANJA KULINDIMA TENA MACHI 26, 2012


Upande wa Jamhuri katika kesi ya kutakatisha fedha haramu inayomkabili Msanii wa Filamu nchini, Kajala Masanja na mumewe Farajja Chambo jana ulishindwa kuleta hati ya mashtaka iliyofanyika marekebisho kama ilivyoamuriwa na mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Dar es Salaam, wiki iliyopita kwa madai kuwa Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP), Dk. Eliezer Feleshi juzi hakuweza kupatikana ofisni kwake ili aweze kutoa kibali.

Wakili wa Taasisi ya Kuzuia na Kupamabana na Rushwa (TAKUKURU), Mussa Hussein, aliikumbusha mahakama mahakama hiyo kuwa kesi hiyo jana ilikuja wa ajili ya upande wa Jamhuri kuleta hati yamashtaka iliyofanyiwa marekebisho, lakini ameshindwa kufanya hivyo kwa sababu juzi, DDP Dk. Feleshi hakuwepo ofisini kwake ili aweze kutoa kibali cha kuletwa hati hiyo mahakamani, kwa hiyo wanaomba wapewe siku moja waweze kutekeleza hilo.

Kwa upande wake Hakimu Mkazi Sundi Fimbo, alikataa hati hiyo isiletwe leo na badala yake, hati hiyo iletwe machi 26 mwaka huu kwa ajili wa washtakiwa kusomewa upya mashtaka hayo na akaamuru mshtakiwa arudishwe rumande, uamuzi ambao ulikubaliwa na wakili huyo wa TAKUKURU na wakili wa Kajala, Alex Mgongolwa.

MAchi 15 mwaka huu, Kajala na mumewe, ambaye pia yupo gerezani anakabiliwa na kosa la utakatishaji fedha haramu katika kesi nyingine, ambako kwa mujibu wa sheria, kosa hilo halina dhamana.


Habari na KajunaBlog

No comments:

Post a Comment