Thursday, March 15, 2012

AIBU YA BOSI


HUWEZI kuamini lakini ndiyo ukweli kwamba, bosi wa kitengo cha ukaguzi wa mahesabu katika idara moja ya serikali jijini Tanga, Olestar ‘amefotolewa’ picha chafu huku akionekana kufurahia, Amani linakupa mkasa mzima.

Licha ya kupiga picha hizo katika mikao tofauti, baadhi ya picha zinamuonesha bosi huyo akiwa mtupu huku mwanaye akiwa pembeni.

Picha zilizotua katika meza ya gazeti hili zinamuonesha bosi huyo akifanya vituko ambavyo si vya kistaarabu ambavyo haviwezi kuanikwa kwa uwazi zaidi gazetini ili kulinda maadili.

Katika picha hizo, pia Olestar alionekana akiwa amevaa nguo vizuri kabla ya kuanza kuingia kwenye majaribu ya kufanya zoezi la kuzisaula moja baada ya nyingine.

Tukio la ajabu, ni kwamba katika moja ya picha hizo, bosi huyo ambaye anakiongoza kitengo hicho nyeti, alionekana akiwa mtupu huku ameshika simu akivalia rozari shingoni.

“ Huu ni upuuzi, mwanamke huyu anaonekana kuwa na heshima zake anayejua dini, hawezi kufanya ujinga kama huu,” alilaani mmoja wa watu waliozushuhudia picha hizo.

Kwa mujibu wa chanzo cha habari, mwanamke huyo alipiga picha hizo kwa lengo la kuziweka kwenye CD na kuwaonesha wanaume pale wanapokwenda nyumbani kwake kupitia runinga.

“ Picha hizo ameziweka kwenye CD ili kuwahamasisha wanaume wanaokwenda nyumbani kwake, huwa anawawekea katika runinga ili wamuone jinsi alivyoumbika na kuwahamasisha kwa ngono,” kilisema chanzo hicho.

Amani liliwasiliana na bosi huyo kwa simu yake ya mkononi ili kupata ufafanuzi wake na kutaka kujua kwa nini amefanya kitendo hicho kilicho nje ya maadili ya Kitanzania.

Alipopatikana, bosi huyo aling’aka kupiga picha hizo, lakini baada ya kubanwa, alikiri na kuahidi kumtuma dada yake katika ofisi za gazeti hili kwa lengo la kuzitambua.

“Mimi najiheshimu sana, siyo malaya kama unavyonifikiria, lakini hata hivyo, inawezekana nitamtuma dada yangu aje hapo ofisini kwenu ili azikague,” alisema.
Hata hivyo, pamoja na kuongeza jitihada za kuwasiliana na bosi huyo, hakuna mtu alionekana katika ofisi za gazeti hili kwa ajili ya kuzitambua picha hizo.

Hatua za mwisho alizochukua bosi huyo ni kuweka mgomo wa kupokea simu za mwandishi wa magazeti ya globalpublisher.

Habari zaidi bonyeza hapa!

Na Issa Mnally, GPL

No comments:

Post a Comment