Monday, February 13, 2012

PATCHO ATISHIWA KUUAWA


MWANAMUZIKI wa Bendi ya FM Academia ‘Wazee wa Ngwasuma’ ambaye pia ni nyota wa filamu Bongo, Patcho Mwamba ‘Tajiri’ (pichani), ametishiwa kuuawa baada ya kutuhumiwa kukwapua mke wa kigogo wa Bandari, Dar es Salaam (jina tunalo).

Kwa mujibu wa chanzo makini, kigogo huyo ameapa kumfanyia Patcho kitu mbaya akimtuhumu kumtongoza mke wake na kuhusika katika kuwakuwadia Wakongo wenzake kwa wake za watu hapa nchini.

“Jamaa ameapa kumwondoa Patcho kwenye uso wa ardhi au kwa usalama wake arudi kwao Kongo (DRC),” kilisema chanzo chetu.

Akizungumzia mkasa huo, Patcho aliliambia Ijumaa Wikienda kuwa baada ya kukutana na vitisho vya jamaa huyo alikimbilia polisi ili kujiweka salama na kwamba hajawahi kufanya kitendo kama hicho.

“Alishanipigia simu na kunitumia meseji za vitisho (huku ‘akizifowadi’ kwa mwandishi wetu), akaniambia nimwache mke wake la sivyo ataniua.

“Unajua mazingira ya kazi yangu ya muziki na filamu inawafanya wanawake wengi kutaka ukaribu na mimi, kinachotokea, mwenye mke akiona hivyo anahisi vingine ‘so’ niko tayari mnikutanishe naye nimweleze ukweli,” alisema Patcho na alipoulizwa kama anamfahamu mke wa jamaa huyo, alisema:
“Unajua ningekutana na huyo jamaa uso kwa uso ningejua ni mwanamke gani lakini ukweli ni kwamba sijawahi kufanya hivyo.”

Habari Na Musa Mateja, GPL

No comments:

Post a Comment