Friday, January 6, 2012

Milovan agoma kula Simba


KUFUATIA kipigo cha mabao 2-1 ilichokipata katika mechi yao ya kwanza katika michuano ya Kombe la Mapinduzi, kwenye mechi dhidi ya Jamhuri ya Pemba, Kocha Mkuu wa Simba, Milovan Cirkovic ‘Profesa Chico’ aligoma kula chakula cha usiku.

Kwa mujibu wa chanzo cha habari kutoka ndani ya klabu hiyo ni kuwa Milovan alichukizwa na matokeo hayo na alionekana mnyonge mara baada ya mechi hiyo, zaidi ni tukio la kuingia ndani na kushindwa kurudi kupata chakula cha usiku na hata alivyofuatwa alitoa jibu kuwa hatoweza kula.

Imeelezwa kuwa ilibidi wamuache huku wakishindwa kumlazimisha ingawa kesho yake asubuhi aliamka akiwa salama na kuweza kunywa chai.

“Kufuatia matokeo ya mchezo wetu dhidi ya Jamhuri siyo tu yaliwachanganya mashabiki wetu bali hata Milovan alishtushwa na matokeo yale, alishindwa kula chakula cha usiku, alivyofika hotelini aliingia ndani hakutoka tena na tulipomfuata kumkumbusha alijibu hawezi kula kabisa,” kilisema chanzo hicho na kuongeza:
“Alipoamka asubuhi alikuwa salama na aliweza kunywa chai kuendelea na programu zake kama kawaida hatua ambayo ilitupa faraja.”

Na Khatimu Naheka, GPL

No comments:

Post a Comment