Timu tajiri Tanzania Bara inayofananishwa na Manchester City huko England, Azam FC, jana usiku imetwaa Taji lake kubwa la la kwanza baada ya kuichapa Jamhuri ya Pemba bao 3-1 katika Fainali ya Mapinduzi Cup iliyochezwa Uwanja wa Amaan, Zanzibar.
Licha ya kutanguliwa bao moja na kukosa penati baada ya mpigaji John Boko kupiga posti ya juu, Azam walipiga bao 3 kupitia Boko, Tchetche na Supastraika Mrisho Ngassa.
Ushindi huo umedhihirisha ubabe na umahiri wa Azam FC walio chini ya Kocha Stewart Hall kutoka Uingereza na Kally Ongala kwani kwenye Mashindano hayo walizigalagaza Yanga bao 3-0 na Simba 2-0.
Mafanikio haya, bila shaka, yatawashitua Vigogo Yanga na Simba na kuwatolea mimacho Azam wakati mzunguko wa pili wa Ligi Kuu Bara utakapoanza hapo Januari 21 hasa kwa vile Azam wako nafasi ya 3 nyuma ya Yanga na vinara Simba.

No comments:
Post a Comment