Monday, January 16, 2012

KITAMBI NOMA BONANZA: YANGA FC vs SIMBA SC hakuna mbabe (0 - 0)

Kikosi cha maangamizi cha watoto wa Jangwani YANGA FC jana kilishuka katika dimba la SUYE P/SCHOOL kumenyana na watani wa jadi SIMBA SC matokeo yalibakia kuwa 0 - 0. Mwanzo mpaka mwisho wa mchezo YANGA ndio walimiliki mpira kwa kiasi kikubwa (asilimia 80%), japokuwa walikosa magori mengi ya wazi kutokana na kutoelewana katika safu ya umaliziaji.

Kikosi cha SIMBA SC kikiongozwa na Hamis Kambi (mfupi mwenye kipara) jana kilishindwa kufua dafu mbele ya YANGA FC....ambapo mchezaji wao wa kukodisha ANDENGISYE alionesha si lolote si chochote baada ya kukosa penati iliyopanguliwa na golikipa wa 'YANGA' Rasta a.k.a Berko. Huku wakiambulia asilimia 20% ya umilikaji wa mpira na kucheza faulo nyingi.

Sheikh Saidi Ngassa alisimamia DUAH vizuri kabisa!

Japo kuwa walikuja na mganga uwanjani na hirizi 45 pamoja na njiwa weupe 12...wekundu wa msimbazi walikumbuka kuwa kuwa Mungu wakapiga duah kabla ya mchezo kuanza.

Hapa ni baada ya mtanange huo kuisha kwa kutofungana (0 - 0) katika viwanja vya Shule ya Msingi Suye...Wekundu wa Msimbazi waligomea penati wakitoa visingizio kuwa kipa wao alikuwa kalewa.


Habari Picha na Mwandishi Wetu - Arusha

No comments:

Post a Comment