Thursday, December 8, 2011


KAULI tata iliyotolewa na baadhi ya wanawake wanaojiuza mitaani usiku, ‘machangudoa’ imeacha mjadala mzito baada ya kuwataja waheshimiwa wabunge kwamba ni miongoni mwa wateja wao wakubwa.

Uchunguzi wa kina uliofanywa na gazeti hili siku za hivi karibuni juu ya biashara hiyo haramu jijini Dar, umebaini siri hiyo nzito ya baadhi ya waheshimiwa wabunge kuwanunua akina dadapoa hao.

Amani, lilifanikisha uchunguzi huo kwa kuzungumza na madadapoa ambao wengi wao walitoboa siri ya jinsi wanavyofanya biashara na wabunge, huku wengine wakitaja majina na tabia zao wawapo ‘kazini’.

Katika majina yaliyotajwa, gazeti hili limejumuisha na kupata jawabu kwamba memba watano wa mjengo wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania (tunawahifadhi kwa sasa) ni miongoni mwa wateja ‘waadilifu’ wa biashara ya ukahaba.

Wabunge hao, wawili wanawakilisha majimbo ya Kanda ya Ziwa, mmoja Kanda ya Kati na wengine Kaskazini Mashariki, wanadaiwa kufika eneo la Afrikasana, Sinza, Dar es Salaam mara kwa mara na kujichukulia machangudoa wa kukesha nao au wakati mwingine kwa ‘short-time’.

Miongoni mwa wabunge hao, mmoja pekee anayetokea Kanda ya Ziwa ndiye kijana, wengine wanne ni watu wazima, huku wawili wakiwa ni wazoefu ndani ya mjengo kwa zaidi ya muongo mmoja.

AMANI MZIGONI
Baada ya vyanzo mbalimbali kutoa taarifa za kuridhisha, gazeti hili namba moja kwa ufutiliaji wa ishu za kijamii, liliingia mitaani na kuzungumza na raia wema kuhusu ufahamu wao kama kuna baadhi ya wabunge wao hutenda dhambi na machangudoa.

Aidha, uchunguzi ulianzia kwa watu ambao walishindwa kathibitisha au kukataa juu ya uwepo wa madai hayo.
“Duh! Unajua huwezi kuthibitisha wala kukataa kwani suala hilo ni la mtu binafsi,” alisema Mama Nancy wa Magomeni jijini Dar.

USO KWA USO NA MACHANGUDOA
Mazungumzo ya kati ya Amani na machangudoa, yalikwenda kama ifuatavyo;
Ashura wa Tandika: “Ni kweli, nani amekwambia ni siri? Mbona ni wateja wetu wakubwa?”
Husna wa Sinza: “Wapo wabunge wanatuchukua kila siku, au unataka tukutajie majina? (akataja ila tumeyahifadhi).”

Sofia wa Buguruni: “Ukweli ni kwamba, waheshimiwa tena wengine wana vitambi vyao wanakuja kutuchukua, tena ni hodari sana kwa ngono tofauti na mwonekano wao.

“Kikubwa ambacho kinawafanya wasitirike na macho ya watu, licha ya giza la usiku, lakini pia magari yao yenye vioo vya giza (tinted) ndiyo kinga yao kubwa.”

Machangudoa hao walizidi kumimina siri nzito zaidi ambapo walisema kuwa ukiachilia mbali wabunge hao wenye vitambi, pia wapo waheshimiwa wenye umri mdogo.
“Yaani usiwaone wana umri mdogo ukadhani wanashobokea mademu wa uzunguni, wao pia ni wateja wetu wakubwa,” alisema Maria wa Kinondoni.

WABUNGE KIZIMBANI
Ili kupata hitimisho la uchunguzi huo, gazeti hili liliamua ‘kujipeperusha’ angani kuwasaka baadhi ya waheshimiwa wa Bunge la Tanzania ili kusikia misimamo yao kuhusu madai ya machangu hao. Pia, kuwauliza kwa nini hawatungi sheria itakayowaondoa makahaba hao barabarani?

Mh. John Komba:
Huyu ni Mbunge wa Jimbo la Mbinga Magharibi(CCM), alisema:
“Unajua (akilitaja jina la mwandishi) wengi wanaochukua machangudoa ni wale wenye fedha kwa maana ya wafanyabiashara wakubwa na wafanyakazi wengine, lakini wabunge sina hakika.”

Aidha, mwandishi wetu alimbana zaidi kwa kumuuliza kama ni fedha mbona hata wabunge wanazo?
“Mh…mmm...aaah unajua hata wabunge si malaika labda kweli wapo, lakini mimi siamini, nadhani ni kutaka kuwachafua majina tu, ninachoona sheria ifuate mkondo wake juu ya hawa makahaba.”

Mbunge wa pili kupandishwa ‘kizimbani’ na gazeti hili ni wa Jimbo la Temeke (CCM) Mh. Abbas
Mtemvu:

“Wao ndiyo wanajua hivyo, unajua hata wabunge ni watu kama wengine, yawezekana ni kweli.”
David Kafulila; yeye ni Mbunge wa Jimbo la Kigoma Kusini (NCCR-Mageuzi):

“Hilo ni suala la aibu na ni siri ya mtu, hivyo siwezi kulizungumzia sana lakini nataka niseme kuwa, siwezi kukataa wabunge hawahusiki maana ni binadamu wa kawaida lakini kama nilivyosema awali, ni jambo la siri mno na aibu.
“Usimamizi wa sheria ni mbovu kwa Tanzania, watu hao (makahaba) walitakiwa wapigwe marufuku.”


Mbunge wa Jimbo la Kinondoni, Mh. Iddi Azzan alisema: “Mh! Unajua kama kuna mbunge anafanya hivyo ni siri yake kwa uwazi hawezi.”
Hata hivyo, kizimba kwa wabunge hakikuishia hapo kwani mwandishi alimtafuta Mbunge wa Jimbo la Ubungo (Chadema), Mh. John Mnyika ambaye aliposomewa mashtaka, badala ya kujibu alidai yuko msibani.

Uchunguzi wa kina unaendelea kufanyika juu ya suala hilo na tutakapokuwa tayari gazeti hili litaanika kila kitu.

Biashara haramu ya uchangudoa inazidi kushamiri kila kukicha hasa katika Jiji la Dar es Salaam, hivyo serikali inatakiwa kuchukua hatua za haraka-Mhariri.

Na Brighton Masalu, GPL

No comments:

Post a Comment