Friday, August 12, 2011

ROSE NDAUKA AMFUNGUKIA WEMA


Na Gladness Mallya
Msanii wa filamu za Kibongo, Rose Ndauka (pichani) ‘amemfungukia’ muigizaji mwenzake, Wema Sepetu akijibu mapigo kufuatia mlimbwende huyo kumtuhumu kuwa alishirikiana na msanii Jacqueline Pentzel ‘Jack wa Chuz’ kumuibia Filamu ya The Diary waliyofanya katika kundi lao la JAROWE.

Akizungumza na Ijumaa jijini Dar es Salaam juzi, Rose aliweka ‘pleini’ kwamba, hawezi kuiba filamu ambayo amechangia nguvu zake kwa asilimia miamoja kwani tangu mwanzo alikuwa anafuatilia kila kitu peke yake huku Wema na Jack wa Chuz wakiwa bize na mambo yao.

Rose alisema kuwa, mara kwa mara alikuwa akiwaambia mastaa hao waongozane ili kuikamilisha filamu hiyo lakini walikuwa wakimpotezea na mpaka sasa haijakamilika.

“ Wema hajawahi kunipigia simu kuniuliza kuhusiana na filamu hiyo na sina ugomvi naye ‘so’ sitaki kusikia maneno, kila mtu ana uhuru wa kufuatilia jinsi kazi yake inavyofanyika.”

Jack wa Chuz, Rose na Wema ni wasanii walioamua kuunda kundi lilikwenda kwa jina la JAROWE ambalo lilidumu kwa muda mfupi na kusambaratika kabla hawajakamilisha filamu hiyo ya kwanza inayoleta mgogoro kwa sasa ambayo hivi karibuni Wema alidai kuwa wenzake wana mpango wa kumpiga changa la macho.

No comments:

Post a Comment