Monday, August 1, 2011

Mmoja afa, 3 hoi hotelini Southern Sun, Dar Es Salaam

Ulevi wa kupita kiasi ndiyo unaosadikika kuwa chanzo cha kifo cha raia mmoja wa Zambia na wengine watatu akiwamo Mtanzania kubaki hoi na mmoja kuzindukia Muhimbili.

Watu hao wanne ambao wote ni wanaume walikutwa katika chumba namba 425 ghorofa ya nne ndani ya Hoteli ya Southern Sun ya jijini Dar es Salaam. Chumba hicho kinadaiwa kukodiwa na raia wa Kiingereza.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ilala, Faustine Shilogile alithibitisha tukio hilo na kusema wanaendelea na uchunguzi.

Aliyezinduka Muhimbili ni Eliud Sikwabi ambaye ni Mwingereza na kuwataja wenzake kuwa ni Ikbar Bahabur wa Zambia na Mtanzania aliyetajwa kwa jina moja la Omari.

Kamanda Shilogile alisema inaonekana kuwa watu hao walikunywa kilevi kupita kiasi. Taarifa zaidi zinasema kwamba watu walianza kunywa katika sherehe ya harusi ya mtoto wa Jaji Mark Bomani, Clement.

source: http://www.wavuti.com/4/post/2011/07/mmoja-afa-watatu-hoi-hotelini-southern-sun-dar-es-salaam.html#ixzz1TlfRcmmb

No comments:

Post a Comment