Tuesday, August 2, 2011

KAMA CHADEMA ITATAWALA NCHI HII, MIMI NITAJINYONGA

Abdallah Zombe akizungumza na wanahabari (picha credit: Victor Makinda)

Na Jiachie blog
Aliyekuwa Kaimu Kamishna wa polisi mkoa wa Dar es Salaam, Abdalah Zombe, amezungumza na waandishi wa habari nje ya Mahakama kuu jijini Dar es Salaam leo asubuhi.

Katika maelezo yake, Zombe alisema kuwa anamshangaa Mbunge wa Arusha mjini, ambaye pia ni Waziri Kivuri wa Mambo ya Ndani, Godbles Lema, kwa kitendo chake cha kuhoji kuhusu uhalali wa hukumu ya Zombe katika kesi iliyokuwa ikimkabili ya mauaji ya wafanyabiashara wa madini kutoka Mahenge. Zombe alisema kuwa Lema, hajui katiba ya Tanzania. Alisema kuwa Lema kama mbunge anapaswa kufahamu kuwa Bunge ni muhimili wa Dola unaojitegemea. Mahakama pia ni muhimili wa Dola unaojitegemea. Hivyo alishangaa kitendo cha Lema (MB) kuhoji maamuzi halali ya Mahakama.

Akiongeza alisema kuwa Wabunge wa CHADEMA hawajui watendalo bungeni na aliapa kuwa endapo Chadema watapata ridhaa ya kuongoza nchi, yeye Zombe atajinyonga. 'Endapo kama CHADEMA watatawala nchi hii, mimi nitajinyonga kabisa' Hiki ni chama cha hovyo na wabunge wake ni wa hovyo. Hawaijui katiba, alisema.


Source: http://www.wavuti.com/habari.html#ixzz1TrFs45pZ

No comments:

Post a Comment