Wednesday, July 20, 2011

WEMA amtumbua shost wake JACK

Na shakoor jongo
‘SHUGAMAMI’ anayetamba kwenye Filamu za Kibongo, Wema Isaack Sepetu ‘amembutulia’ mbali shoga yake, Jacqueline Pentzel ‘Jack wa Chuz’ kutokana na shinikizo la familia yake.

Akizungumza na Risasi Mchanganyiko nyumbani kwa shoga yake mpya, mshiriki wa Miss Kiswahili, Rehema Fabian Kinondoni jijini Dar es salaam, Wema alisema kuwa ameamua kusikiliza ushauri wa familia yake ili kuepukana na skendo za mara kwa mara.

“Ukitaka kuishi vizuri katika dunia uwe tayari kusikiliza ushauri kutoka kwa watu waliokuzidi umri, sasa nimeamua kufanya hivyo na hali imekuwa shwari,” alisema Wema.

Wema amesema, tangu alipofuata ushauri huo, hajakumbana na skendo ya aina yoyote ile.
Baada ya Wema kusema yake, gazeti hili liliwasiliana na Jack wa Chuz ambaye alidai kuwa alichoshwa na maneno ya mama mzazi wa Wema.

“Siyo kama tuna bifu au hatuna mawasiliano, maneno ya mama yake eti ninamharibu mtoto wake yamenichoma sana, nimeona nijiepushe lakini sina ugomvi na Wema,” alisema.

Jack alisema kuwa alipata ushauri kutoka kwa watu mbalimbali kwamba awe mbali na Wema kutokana na kauli ya mama yake.

“Kitu kimoja nataka nikuambie, kwani mimi ndiye niliyemtuma Wema akamtukane Bob Junior? Au mie nilikuwepo wakati akimtukana Rehema (Fabian)? Kadaiwa kuiba simu mi nilikuwa naye?” Alihoji.

Hata hivyo, Jack alisema yeye alikuwa akifuatana na Wema kwenda polisi na mahakamani kwa ajili ya kumsapoti tu lakini hatimaye amekuja kuonekana mbaya.

“Nashukuru kwa yote, naendelea na mambo yangu lakini kwa kifupi nimeamua kuachana na Wema kutokana na kauli ya mama yake,” alisisitiza Jack.

Mama mzazi wa Wema, Miriam Sepetu, aliwahi kuripotiwa akimtaja Jack wa Chuz kuwa ndiye chanzo cha mwanaye kuingia kwenye skendo za ajabu.

SOURCE: GPL

No comments:

Post a Comment