Waziri kivuli Wizra ya Mambo ya Nchi za Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Ezekia Wenje ambaye pia ni mbunge wa Nyamagana jana asubuhi alitolewa nje na mwenyekiti wa mkutano wa nne kikao cha thelathini na nne, Slyvester Mabumba wakati alipoingia kutaka kutoa hoja ya kuahirishwa kwa Bunge kwa
maslahi ya Taifa.
Kutimuliwa kwa Waziri huyo kulifanyika muda mfupi baada ya majibizano ya muongozo wa spika kati ya Mwenyekiti na Mbunge wa NCCR- Moses Machale, Mbunge wa Kasulu Mjini kufuatia hoja iliyotolewa na mbunge Tundu Lissu kuhusu uwongo alioutamka Naibu Waziri Kassim Majaliwa (Elimu-TAMISEMI kuhusiana na michango ya wananchi.
Mtafaruku huo ambao ulikuwa umejengewa hoja ulionesha ubinadamu unavyotumika katika maamuzi na utendaji na oda zinazosytahili kufuatwa. kutokana na mazingira ja majibizano ya awali inaonekana hoja ya Wenje iliungwa na mtafaruku uliokuwa ukiendelea ambapo alikuwa anataka kutoa taarifa na hivyo Mwenyekiti kutoa amri ya kutolewa nje.
Kwangu mimi (Msimbe) hoja nzuri ya Wenje ilimezwa na fikira za kibinadamu badaa ya majibizano ya kaa chini na mimi lazima niseme licha ya Waziri Lukuvi kusema kwamba hoja ni ndogo na haihitaji kukuzwa.Baada ya Wenje kutoka baadhi ya Wabunge nao walitoka na nje nusura mwingine achapwe vibao baada ya kusema "nyie wajinga".Pale nje Wenje alisema kwamba anashauri "Spika ampeleke shule mwenyekiti wa mkutano ili ajue namna ya kuwa sober".Naam, bunge limechemsha unaweza kujiuliza nani kachemsha Mwenyekiti au Waziri au wote? Naam hili ndilo Bunge! Watoke... Tokeni... Oda... Sikiliza nyie...
No comments:
Post a Comment