Thursday, July 28, 2011

Miss Progress avimba mwili mzima


Na Gladness Mallya
Miss Progress International 2010/11, Julieth William (pichani), amekumbwa na ugonjwa wa kuvimba mwili mzima baada ya kumeza dawa za malaria.

Akizungumza na ‘vuvuzela’ wa Amani aliponaswa katika Hospitali ya TMJ jijini Dar es Salaam juzi, Julieth aliweka ‘plein’ kwamba, alitimba hospitalini hapo baada ya kuona hali inazidi kuwa mbaya na zaidi mwili ulikuwa ukimuwasha kupita maelezo.

“Nilikuwa na malaria kali sana, nikameza vidonge vya Artequin, nashangaa dawa hizo zimenifanya vibaya, yaani nikivua nguo utakimbia. Nimekuja hapa hospitalini kuchoma sindano ya kuondoa sumu mwilini, namshukuru Mungu naendelea vizuri, japo bado sijapona,” alisema Julieth.

Julieth anatumikia taji hilo akiwa na mradi wa kuwasaidia walemavu wa ngozi (albino) aliouanza Novemba 2010, ambao utamalizika Novemba 2011 huku akiwa ameshawatembelea watu hao katika mikoa mbalimbali ikiwemo Dar es Salaam, Arusha, Mara na Mwanza.

No comments:

Post a Comment