Na Global Publishers Tz
Catherine Magige Mbunge wa Viti Maalum kupitia tiketi ya Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) akitokea Mkoa wa Arusha, ametoa sapoti ya fedha ili kufanikisha Shindano la
Jenga Nchi Yako (JNY).
Mratibu wa shindano hilo, Richard Manyota mwenye ‘taito’ ya Balozi wa Amani na Ulinzi Shirikishi Vijana Taifa, aliliambia gazeti hili juzi (Jumatano) kwamba, Mheshimiwa Magige ameahidi kuchangia kiasi cha shilingi 500,000.
“Kuwasaidia vijana waweze kujiajiri ni jambo la muhimu sana, litasaidia kuondoa matatizo mengi kwenye jamii,” alisema Magige ambaye ni mbunge wa pili kuchangia shindano hilo baada ya Mhe. Ahmed Shabiby (Gairo) kuahidi kiasi kama hicho hivi karibuni.
Lengo la JNY ni kuwasogeza vijana karibu hasa walioko vijiweni na kuwahamasisha kuhusu kujiajiri kupitia vipaji vyao, kupandikiza mbegu ya uzalendo ambapo washindi watakaopatikana wataunda kundi jipya la muziki wa kizazi kipya litakalodhaminiwa kurekodi nyimbo mbili katika Studio za Tatoo Record zilizopo Masaki, Dar.
No comments:
Post a Comment