Tuesday, July 26, 2011

Faza Nelly: Nuru ya Hip Hop iliyozima na Kupigwa Kisu


Jumatatu ya 29 March Mwaka 2006 Fans wa Swahili Hip hop World wide dunia nzima walikua na simanzi kutokana na Taarifa za kifo cha Nelson Chrizostom Rutta/maarufu kama Faza Nelly ambae alikufa kutokana na Majeraha ya kuchomwa na Kisu mara tisa na Jirani yake akijulikana na kama Moses Yohana Kilevo,

Baadhi ya watu watakua wanajiuliza Faza Nelly ni nani? Kuna majibu mengi katika swali hilo, lakini Jibu Katika Music Industry ni kwamba Faza Nelly ni Mwanzilishi wa kundi la XPlastaz, Kundi la Rap kutoka A-town ambalo lilikua na Memberz sita wengi wao wakiwa ni ndugu, kundi lilijilikana world wide kupitia Concert tours walizofanya Brazil, Holland, U.K na sehem nyingine duniani without forgetting their Mama land Tanzania, na umaarufu wa X-Plastaz unatokana na kwamba walikua wakitumia Hardcore Beats, Swahili Rhymes na Traditional Maasai Music ambayo huimbwa na Maasai Warrior akiitwa Merege, Memberz wa X-plastaz ni Ziggy Lah, G Ssan,Steve, MeregeDiney na The late Faza Nelly,

Kifo cha Faza Nelly

Kama nilivyosema mwanzo mchizi aliyehusika na Mauaji ya Faza Nelly alikua ni jirani yake moses yohana Kilevo, Jirani huyo alikua na Historia ya kuwatishia jirani zake siku zote kama vile kuandika kwenye Kuta za kitaani kwao kuwa yeye ni muuaji/ Iam a Killer bila kujali hata watoto wake wanaona maandishi hayo na inaweza kuwaathiri watoto hao…

Mambo kama hayo ya kutokueleweka kwa Jirani huyo yaani Moses Yoahana Kilevo yalisababisha majirani wote kuungana na Kusgn barua ya kuomba kwa serikali ya mtaa kum’hamisha kitaani hapo kwa kilicho elezwa kuwa hawana imani nae kutokana na vitisho vya kuua alivyokua anavitoa kwa wenzake mara kwa mara,,,,,

Kuna siku moja, mmoja kati ya rafiki wa Faza Nelly ambae alikua akiishi nyumba moja na Faza Nelly na Moses Pia, anaitwa Musa alijaribu kuongea na muuaji lakini baadae akaja kukamatwa na Polisi kwa tuhuma za uongo za kumkaba na Kumwibia Moses, kitu ambacho hakikuwa kweli, Faza Nelly akajaribu kumtetea Musa polisi kuwa si mwizi, na kuelezea ukweli juu ya uzushi ule na kwamba hata

Majirani wote wanalijua hilo, ndipo polisi wakamwambia basi aende na Majirani kutoa ushahidi, Faza Nelly akarudi home na kujaribu kuzungumza na Muuaji Moses ambae alikasirishwa na Tukio hilo na kutaka kupigana na Faza Nelly, ili kuepusha ugomvi Nelly aliamua kurudi chumbani kwake, kulala, sekunde chache baadae Muuaji Moses akamjia na Kisu kisu kikubwa na Kumchoma nacho Faza nelly Sehemu tofauti za mwili wake mara Tisa, ikiwemo puani, begani na Kwenye Mapafu.

Kwa mujibu wa familia yake na Mazingira, inasemekana hakukua na Mapigano kabisa katika Tukio hilo, Na Faza Nelly alikua ni Mtu amani/ mpole, Mkarimu ambae hakuweza kumdhuru mtu yeyote, na hii ilijidhihirisha kwenye Lyrics zake kama katika Tittle ya ngoma yake inaitwa NINI DHAMBI KWA MWENYE DHIKI, na ndio maana hata aliposhambuliwa na Muuaji Moses Kilevo alishindwa kujitetea, ukizingatia pia alishambuliwa kutoka mgongoni,

Baada ya Tukio hilo Nelly akaspend siku mbili Hospitalini akiwa anatumia mashine za kupumulia, madaktari walijaribu kuokoa maisha yake lakini walipotaka kumfanyia Surgery kwa mara ya pili, ghafla hali yake ikawa mbaya sana na kufariki mbele ya madaktari na Rafiki yake Musa.

Muuaji…Moses Yohana Kilevo

Alikua ni baba wa familia ya watoto wawili na mke mmoja, alikua ni mtu timamu yaani hakua kichaa, na alijulikana kwa vitendo vyake vya vitisho kwa majirani zake, hakua mstaarabu kabisa, baada ya tukio hilo la kikatili Muuaji huyu alikimbia na hajaonekana mpaka leo, Polisi bado wanafanya upelelezi na kuna uwezekano mkubwa kuwa alikimbilia Nairobi kwani huko ana ndugu, kipindi kile familia ya Faza Nelly iliweka laki tano kwa mtu yeyote atakaye fanikisha kukamatwa kwa muuaji huyo.

Mazishi

Mazishi ya The late Faza Nelly yalifanyika siku tano baada ya kifo chake, na kuchelewa kwa mazishi yake kwa kuwa Familia yake ilibidi kumsubiri mdogo wake Faza Nelly, anaitwa G-San ambaye anaishi nje ya Nchini Markeani, na soon as alpofika Arusha, hatimaye mwili wa Faza Nelly ukahifadhiwa katika Makaburi yaliyopo Njiro Arusha, zaidi ya watu elfu moja walimzika Mwana hip hop huyu, vijana kwa wazee, simanzi ilitawala Katika Ulimwengu wa Hip Hop, Mungu ailaze roho ya marehemu mahala pema.

Mungu ailaze Roho ya Faza Nelly mahali pema peponi…Amen


Na Clouds Media

No comments:

Post a Comment