Habari kutoka Moshi Mkoani Kilimanjaro zinapasha (blogu za Lukwangule na Mroki) kuwa ajali mbaya imetokea katika eneo la Kibosho Road Wilayani Moshi vijijini na kupukutisha maisha ya Watanzania 11 na kujeruhi wengine 26.
Chanzo cha ajali kinatamkwa kuwa ni mwendo kasi na dereva wa basi alikuwa amelewa chakari.
Mabaki ya magari mawili aina ya Fuso lenye namba za usajili T 884 BFL na basi la abiria mali ya kampuni ya Lim lenye namba za usajili T 489 BJR zilizogongana uso kwa uso yanaonekana kwenye picha hapo.
source: http://www.wavuti.com/4/post/2011/07/ajali-yaua-11-moshi-kilimanjaro.html#ixzz1TaAhso1e
No comments:
Post a Comment