Monday, June 18, 2012

TNTz: MMILIKI WA NYUMBA YA WEMA HUYU HAPA



Siku chache baada ya msanii mwenye vibweka vingi ndani ya tasnia ya filamu Bongo, Wema Abrahamu Sepetu kutangaza kuwa anamiliki mjengo wenye thamani ya shilingi za kibongo Ml 400, hatimaye mmiliki halisi wa mjengo huo ameibuka.

Akizungumza na Teentz.com mapema leo,mmoja watu walio karibu na mmiliki huyo mwenye asili ya kiarabu anayemiliki jina la Ahmed au Msafiri kama anavyojulikana kwenye mitaa hiyo amesema kuwa Wema aliutangazia umma juu ya umiliki wake kwa nyumba hiyo wakati ambao kijana huyo wa kiarabu alikuwa safari nchini Brazil kwenye michongo yake.

“Unajua Wema amewadanya watu kwa kiasi kikubwa, nafikiri anatakiwa kuomba radhi nakuwaeleza ukweli kwenye nyumba ile hana hata kipande cha tofali na mmiliki halisi ni mshikaji wangu Ahmed ambaye mara kadhaa huwa anasafiri kwenda nchini Brazil kibiashara” kilisema chanzo hicho.

Dismas Ten

No comments:

Post a Comment