MTU mmoja (mwanaume) ambaye jina lake halikupatikana mara moja aliyekuwa akiendesha gari ndogo aina ya Toyota (Baloon) lenye namba za usajili T630 AED, Jumapili iliyopita alinusurika kifo baada ya ya kugonga miti na garhilo kuharibika vibaya upande wa mbele mjini Morogoro.
Mtu huyo ambaye kwa sasa amelazwa kwenye chumba cha wagonjwa mahututi Hospitali ya Mkoa wa Morogoro,alikuwa akitoka kustarehe katika klabu ya 4 Stars ambapo aligonga mti wa mwembe.
Mtandao wetu ulipofika hospitalini hapo ilishindikana kuongea na majeruhi huyo kutokana na hali yake mbaya na kwamba alikuwa pekeyake kwenye gari.
Mwembe huo mwaka 2006 mtandao huu ulipiga picha ya mtoto wa kigogo wa Chuo cha Ujenzi Mkoa wa Morogoro aliyapoteza maisha baada ya kuugonga mti huo, na mwaka 2007 Meneja wa Mkuu wa Hotel ya Front View iliyopo naebei ta Msamvu aligonga mti huo na kufa hapohapo alipokuwa akitoka maeneo ya Liti kuwarudisha wafanyakazi wake.
Vilevile, mwaka jana madereva wawili wa ‘bodaboda’ pia waligonga mti huohuo na mmoja alifariki dunia huku mwingine akinusurika ingawa alipata kilema cha maisha
NA DUNSTAN SHEKIDELE, GPLMOROGORO
No comments:
Post a Comment