Thursday, June 14, 2012

AY KUFANYA VIDEO NYINGINE YA MILIONI 30 SOUTH AFRICA?


Ni swali ambalo jibu lake ninalo tayari, AY ambae jumapili ya weekend hii ataivunja rekodi ya kuwa mtanzania wa kwanza kuperform kwa mara ya pili kwenye stage ya Big Brother Africa ameamplfy Exclusive kwamba kuna uwezekano akaitumia hiyo nafasi kufanya video nyingine ya pili.

Ni wiki mbili zimepita toka atoke huko huko South Africa alikokwenda kufanya video yake ya kwanza yea gharama kubwa ya milioni 30 iliyofanya na kampuni ya Godfather ambayo imefanya video nyingi za kina P Square, J Martins, Mr Flavour na wengine.

Ay ambae ameshine kwenye mikataba minene ya matangazo ya Vodacom aliyofanya zamani huku sasa hivi akiwa na mkataba wa matangazo ya Airtel ameamua kuwekeza sehemu ya pato lake kwenye video zenye ubora wa kimataifa kwelikweli time hii.

Amesema sasa hivi wanachonga script ya hiyo new video ya single ambayo bado hajawa tayari kutaja jina lake kwa sababu bado hajaisajili BASATA lakini ni single aliyomshirikisha Vannesa Mdee mtangazaji wa Choice Fm 102.6 Dar es salam.

Video ya kwanza ilimgharimu Ay shilingi milioni 30 na hii ya pili pia itakua ni Milioni 30 kama kawaida, Nilipomuuliza Ay kama haoni kuna hasara kwenye hizo milioni 60 za video mbili, amesema “hii ni biashara na biashara yoyote ni lazima uwekeze hakuna faida inayokuja tu bure bure, watu ni uoga tu ujue wa kuwekeza wanabaki kuelekeza vidole kwa Wanigeria ambao wanawekeza pesa kwenye muziki, mimi najibana pia ninachokipata nakigawa.. hata zamani ilikua hivi hivi tu watu walikua wanashangaa Ay unakwenda Uganda unapoteza hela, leo hii wao wanahangaika kwenda Uganda na Kenya mimi nimeshatoka huko”

Ay anaondoka bongo jumamosi kwa ajili ya kwenda kuperform Big Brother jumapili akiwa kwenye stage moja na wakali wa kenya Sauti Sol.

Source: MillardAyo

No comments:

Post a Comment