Tuesday, February 21, 2012

Mama wa mtoto huyu ni katili


MTOTO anayekadiriwa kuwa na umri kati ya miaka miwili hadi mitatu ambaye jina lake halikuweza kujulikani, amefanyiwa ukatili na mama yake baada ya kutupwa na kuokotwa katika shilo la takataka jirani na reli, Buguruni jijini Dar es Salaam.

Waliomuokota mtoto huyo ‘malaika’, aliyetelekezwa na mama yake ni Polisi wa Kituo cha Buguruni, Dar es Salaam na tayari ameshapelekwa katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili.

Akizungumza na mwandishi wetu wiki iliyopita
Afisa Ustawi wa Hospitali ya Taifa Muhimbili, Mariana Kasili alisema kwamba mtoto huyo alifikishwa hospitalini hapo na muunguzi wa Hositali ya Amana aliyejitambulisha kwa jina la Fatuma Mussa ambaye alisema alikabidhiwa na polisi wa Buguruni.

“Mtoto huyu tunaye hapa tangu Februari 12, mwaka huu na haongei vizuri, hakuna aliyejitokeza kumtambua, amekuwa akilia mara kwa mara akiwataka wazazi wake, waliopotelewa au wanaomjua wawasiliane na ofisi hii,” alisema Mariana.


Na Makongoro Oging' - Uwazi, GPL

No comments:

Post a Comment