Monday, January 9, 2012

TUZO ZA FIFA UBORA DUNIANI: Washindi kujulikana leo!


Leo usiku huko Zurich, Uswisi Washindi wa Tuzo za Mchezaji Bora Duniani, Kocha Bora Duniani na Goli Zuri Duniani kwa Mwaka 2011 atajulikana katika hafla maalum.

Pamoja na Tuzo hizi kwa Wanaume pia Kinamama watawania Tuzo zao.

FIFA Ballon d’Or, ‘Mpira wa Dhahabu’==MCHEZAJI BORA DUNIANI
Wagombea wa Tuzo hii ni Wachezaji watatu, ambao wote wanachezea Spain kwenye La Liga, na nao ni Lionel Messi, Cristiano Ronaldo na Xavi.

Hii Tuzo ya FIFA Ballon d’Or ilianzishwa Mwaka jana na huendeshwa na FIFA pamoja na Gazeti la Ufaransa la Soka liitwalo ‘France Football’ kufuatia kuunganishwa Tuzo ya FIFA ya Mchezaji Bora Duniani, iliyokuwa ikiendeshwa na FIFA na Ballon d’Or, iliyokuwa ya France Football.

Jopo litakalochagua Mshindi wa Tuzo hiyo litakuwa ni mchanganyiko wa Waandishi wa Habari wa Kimataifa na Makocha wa Timu za Taifa na Makepteni wao.

Messi ndie alietwaa Tuzo hii ilipoanzishwa kwa mara ya kwanza hapo Mwaka jana na pia alitwaa Tuzo ya Mchezaji Bora Duniani Mwaka 2009.

Cristiano Ronaldo, ambae sasa ni Mchezaji wa Real Madrid, alishinda Tuzo hiyo Mwaka 2008 wakati akiwa na Manchester United.

Ikiwa Messi ataitwaa tena Tuzo hii ataungana na Kiungo wa zamani wa France Michel Platini na wale Magwiji wa Uholanzi, Johan Cruyff na Marco van Basten, kwa kuwa Wachezaji pekee kuichukua mara tatu.

Kocha Bora Duniani
Wagombea wa Tuzo ya Kocha Bora Duniani ni Pep Guardiola wa Barcelona, Bosi wa Real Madrid Jose Mourinho na Meneja wa Manchester United Sir Alex Ferguson.

Wagombea Goli Zuri la Mwaka
Wale watakaowania Tuzo ya FIFA iitwayo Puskas kwa Mchezaji aliefunga Goli zuri la kuvutia kwa Mwaka 2011 ni Lionel Messi (Argentina), Neymar (Brazil) na Wayne Rooney (England).

Washindi wa zamani wa Ballon d'Or:
1956 - Stanley Matthews
1957 - Alfredo Di Stefano
1958 - Raymond Kopa
1959 - Alfredo Di Stefano
1960 - Luis Suarez
1961 - Omar Sivori
1962 - Josef Masopust
1963 - Lev Yashin
1964 - Denis Law
1965 - Eusebio
1966 - Bobby Charlton
1967 - Florian Albert
1968 - George Best
1969 - Gianni Rivera
1970 - Gerd Mueller
1971 - Johan Cruyff
1972 - Franz Beckenbauer
1973 - Johan Cruyff
1974 - Johan Cruyff
1975 - Oleg Blokhin
1976 - Franz Beckenbauer
1977 - Allan Simonsen
1978 - Kevin Keegan
1979 - Kevin Keegan
1980 - Karl-Heinz Rummenigge
1981 - Karl-Heinz Rummenigge
1982 - Paolo Rossi
1983 - Michel Platini
1984 - Michel Platini
1985 - Michel Platini
1986 - Igor Belanov
1987 - Ruud Gullit
1988 - Marco van Basten
1989 - Marco van Basten
1990 - Lothar Matthaeus
1991 - Jean-Pierre Papin
1992 - Marco van Basten
1993 - Roberto Baggio
1994 - Hristo Stoichkov
1995 - George Weah
1996 - Matthias Sammer
1997 - Ronaldo
1998 - Zinedine Zidane
1999 - Rivaldo
2000 - Luis Figo
2001 - Michael Owen
2002 - Ronaldo
2003 - Pavel Nedved
2004 - Andriy Shevchenko
2005 - Ronaldinho
2006 - Fabio Cannavaro
2007 - Kaka
2008 - Cristiano Ronaldo
2009 - Lionel Messi
2010 - Messi


Na Soka In Bongo

No comments:

Post a Comment