Wednesday, December 14, 2011

TFF kuwajadili Mkwasa, Julio


SHIRIKISHO la Soka Tanzania (TFF), limesema linatarajia kuijadili timu ya taifa ya Bara, Kilimanjaro Stars, iliyokuwa ikifundishwa na makocha, Boniface Mkwasa na Jamhuri Kihwelo ‘Julio’.

Akizungumza na Championi Jumatano, Ofisa Habari wa TFF, Boniface Wambura, alisema wanasubiri ripoti ya makocha hao kabla ya kukaa chini kwa lengo la kutafuta uamuzi juu ya nini cha kufanya baada ya timu hiyo kufanya vibaya katika michuano ya Chalenji.

“Kwa sasa hatuwezi kusema kitu chochote hadi pale makocha, Mkwasa na Julio, watakapowasilisha ripoti na kuelezea tatizo lilikuwa wapi mpaka timu hiyo ikashindwa kuchukua hata nafasi ya tatu.

“Kwa ujumla matokeo hayo hayakumfurahisha mtu na kila mmoja alipenda tufike mbali na ikiwezekana tuchukue ubingwa lakini hatuwezi kuamua lolote bila kuwasikiliza makocha,” alisema Wambura.


Na Khadija Mngwai, GPL

No comments:

Post a Comment