Thursday, November 17, 2011

Shoo ya Sugu na Vinega Ustawi yabamba kitaa


KITAA kimechafuka na kila mtu kwa sasa haambiwi kitu kuhusu shoo ya Burudani kwa Mashabiki, Muziki Unalipa ambayo itafanyika Novemba 26, 2011 kwenye Uwanja wa Ustawi wa Jamii, Kijitonyama, Dar es Salaam.

Shoo hiyo, ‘itagemuliwa’ na Mbunge wa Mbeya Mjini (Chadema), Joseph Mbilinyi ‘Sugu’, huku wakongwe Haroun Kahena ‘Inspector Haroun’ na Karama Bakari ‘Luteni Kalama’ wakiwa na dhamira ya kuthibitisha kwamba Gangwe Mob Bongo jukwaani ni sawa na G Unit Marekani.

Shujaa wa Kundi la Wagosi wa Kaya, Fred Maliki ‘Mkoloni’, Anselm Ngaiza ‘Soggy Dog’ na mwana Hot Pot Family mwenzake, Suma G, Mapacha, Dani Msimamo, G Solo, Rama Dee, Peen Lawyer, Adili Mkwela ‘Hisabati’, D wa Geto, Magazijuto, Coin, LWP ‘Majitu’ na wengine kibao.

Uchunguzi umebaini kuwa gumzo kuhusu shoo hiyo imeshika mbaya kitaani, huku ubunifu wa matangazo na viwango vya Vinega wa Anti Virus vikiwa ni kielelezo cha kumfanya kila Mtanzania aone tamasha hilo si la kukosa.

Mratibu wa shoo hiyo, Mkoloni anapatikana kwa namba 0719 690 100, hivyo maelezo kuhusu utaratibu wote kwa jumla, yanapatikana kwake.


Na GlobalPublishersTz

No comments:

Post a Comment