Thursday, November 24, 2011

KONA YA MKUBWA KAMBI: JE, mwaweza kuoana dini tofauti? USIJIDANGANYE!


Kwanza
Fikiria wewe ni mkulima na unataka kutumia jembe la kukokotwa na ng’ombe kwa ajili ya kulima shamba. Kwa kuwa una Ng’ombe mmoja (dume) na Mbuzi mmoja (beberu) unaamua kuwafunganisha nira (yoke) ili uwatumie kukokota jembe na shamba lilimwe.

Ukweli huu ni uvivu wa kufikiri na ni kutaka kusababisha maafa.
Anyway mtu yeyote mwenye akili timamu atajua ubongo wako una matatizo kwani haijawahi tokea mbuzi na ng’ombe wakafungwa nira pamoja na shamba likalimwa.

Linapokuja suala la ndoa au mahusiano wapo watu ambao huamini kufungwa nira pamoja na mtu wa imani tofauti haina tatizo kama kwa ng’ombe na mbuzi kufungiwa nira moja na tayari kwa kulimba shamba.

Pili
Kawaida ikiona kuna alama ya NO EXIT kuingia humo lazima ufikiria mara mbili Kitendo cha kutoa ahadi kwamba Hadi kifo kitakapotutengenisha ukweli binadamu unakuwa ume –launch moja ya ahadi za pekee duniani.
No turning back, no escape route kulia au kushoto, wawili mnaingia kwenye life boat, hakuna kwa kwenda zaidi ya kubaki na huyo umemkubali.

Ukweli ni kwamba mtu mwenye akili timamu akiambiwa nyumba unayoingia haina EXIT atafikiria kwa makini zaidi na zaidi ya mara mbili.

Kazi yako ipo well defined hakuna kutoka, hapa nazungumzia mtu ambaye kweli yupo serious kwanza kuhakikisha ndoa yake inampa Mungu utukufu .
Na kwamba suala la dini na imani ni muhimu sana kwake otherwise hakuna shida.
Mambo ambayo wakati mwingine huleta shida sana kwenye ndoa ni dini, rangi (race) na taifa hata hivyo linaloweza kuwa mwiba mkali ni suala la dini.

General rule ni kwamba “The more couples have in common the better the chance of success”

Ukweli unabaki palepale kwamba waumini wa kweli wa dini tofauti (let say muislam wa swala tano na mkristo aliyeokoka) wakioana kuna uwezekano mkubwa kukumbwa na matatizo yanayohusiana na dini katika ndoa yao.
(Najua ukianza kuzungumzia dini unaweza kuwasha moto ambao kuzima ni ngumu hata hivyo lazima kuongea ukweli)

Watu ambao hupuuza hiki kipengele baada ya kuoana wanayo ya kusimulia kwa masikitiko.
Jambo la msingi kabla ya kuoa au kuolewa ni vizuri kupata solution ya suala la dini au suala la imani, usijidanganye kwamba mkioana utanyoosha kwa pasi ya umeme kirahisi suala la hili la dini, hapa unahitaji kuwa genius tumia akili zako zote kuhakikisha umejua nini hatima yake.

Unaweza kuvuka mito mingi tu lakini mto wa dini ni lazima uvuke ukiwa makini kabisa maana unaweza kuzama mbele ya safari.

Je, mtasali wapi na kivipi, na watoto wakizaliwa watakuwa dini gani na dini ya mwenzako ina amini vipi kuhusu ndoa?
Ni maswali ya msingi sana.

Wengi huona hii ni issue ndogo sana na tutakabiliana nayo tukiona sasa muhimu ni love maana nampenda kuliko suala la dini.
Ukweli vitu vidogo ndo hupelekea ndoa kwenda shimoni.
Na kuacha kujadili sasa haiwezi kumaliza tatizo baadae, kumbuka
“the sooner the better”
au niseme
“the more you solve now the greater your compatibility later.

Imani ya dini ni moja ya njia mke na mume huwa connected, dini ni big deal na zaidi ili ndoa iwe strong haina budi kuwa na 3 layers yaani connection ya kimwili, kihisia (emotions) na kiroho na bond ambayo hushika ndoa (siyo sex) mara nyingi ni kiroho.

"Marriage is not a trial like foreign dish sampled to see if it is tasty"


Na Mkubwa Kambi (Maisha na Ushauri)

No comments:

Post a Comment