Friday, October 21, 2011

GPL: MAJIBU YA UKIMWI YA WOLPER, SINTAH YANASWA



LICHA ya watu wengi kuficha majibu yao baada ya kupima na kugundulika wanaishi na Virusi Vya Ukimwi, gazeti namba moja kwa kuandika habari za mastaa Bongo la Ijumaa, limenasa majibu ya wasanii maarufu wa filamu, Jacqueline Wolper na Christina Manongi ‘Sintah’.

Kunaswa kwa majibu ya mastaa hao kumetokana na vijimaneno vya watu ambao walikuwa wakisambaza uvumi kuwa, masistaduu hao wana miwaya.

Kufuatia uvumi huo, hivi karibuni paparazi wetu aliwatafuta mastaa hao na kuwahoji juu ya kilichokuwa kikisemwa mitaani kuhusu afya zao ambapo walikiri kusikia ila wakasema ni maneno ya watu tu.

“Wanaosema hivyo ni maadui zangu ambao hawapendi kuona nikifanikiwa, kwa taarifa yao sina ngoma na kukuthibitishia hilo nipo tayari kwenda kupimwa hata sasa hivi,” alisema Sintah.

Baada ya mwandishi wetu kuambiwa hivyo, alimwendea hewani Wolper na kumshawishi kama anaweza kwenda kupima ambapo alisema atakachokifanya atamletea cheti cha majibu yake.

“Mimi nimepima wiki mbili zilizopita, ngoja nikuletee majibu yangu,” alisema Wolper.
Kama alivyoahidi, haukupita muda mrefu Wolper alifika Kinondoni alipokuwa mwandishi wetu na kumuonyesha cheti alichopima ukimwi Septemba 28, 20011.

Baada ya paparazi wetu kuona cheti hicho, aliongozana na mastaa hao hadi Hospitali ya Mama Ngoma iliyopo Mwenge ambapo Sintah naye alipima damu yake na kuonekana yuko salama.

Hivi karibuni kuna baadhi ya watu wamekuwa wakivumisha maneno kwamba mastaa fulani wanaishi na VVU kwa nia ya kuwachafua jambo ambalo siyo zuri.


Na Imelda Mtema

No comments:

Post a Comment