Wednesday, August 10, 2011

Shindano la kumsaka TOP MODEL wa Vodacom Miss Tanzania

Baadhi ya warembo wa Vodacom Miss Tanzania ambao hawakufanikiwa kuingia
katika Fainali wakiwa wameketi. Mshindi wa taji la TOP MODEL atajinyakulia tiketi ya moja
kwa moja ya kuingia Nusu Fainali ya Vodacom Miss Tanzania 2011.

Warembo 5 kati ya 30 wanaowania taji la Vodacom Miss Tanzania 2011, ambao wamefanikiwa kuingia fainali za kusaka taji la TOP MODEL wakiwa wamejipanga mbele ya majaji baada ya kufanikiwa kuingia katika hatua hiyo usiku wa Agosti 9,2011 katika Hotel ya Giraffe Ocean View jijini Dar es Salaam.

Majaji wa shindano hilo wakiumiza vichwa kutafuta mshindi. Warembo wote walikuwa wakati lakini 1 ndo anahitajika. Mshindi wa TOP MODEL anataraji kutangazwa leo katika siku maalum ya Waandishi Wa habari kufanya mahojiano na Washiriki hao wa Vodacom Miss Tanzania katika Hoteli ya Giraffe.


...washiriki wakipita mbele ya majaji


Habari Picha na Othman Michuzi, Mtaa Kwa Mtaa

No comments:

Post a Comment