Wednesday, August 3, 2011






Neno mcharuko ndilo linalotosha kusindikiza tabia ya staa wa filamu Bongo, Elizabeth Michael ‘Lulu’, kutokana na vioja vya kiwango cha juu alivyofanya Moshi, Kilimanjaro wiki iliyopita.

Lulu, alikwenda Moshi na mastaa wenzake wa Bongo Movie Club kwenye tamasha moja kuelekea miaka 50 ya Uhuru, wakiwa kwenye Viwanja vya Hugo, ‘bi mdogo’ huyo alimwaga ‘lazi’ baada ya kuchizika kwa sebene.

Bendi ya African Stars International ‘Twanga Pepeta’, ilihusika vilivyo ambapo Lulu alipoitwa jukwaani ‘kusugua kisigino’, yeye alisasambua mithili ya Kundi la Welawela.

Dakika nne ambazo Lulu alizitumia kufanya kweli jukwaani, zilitosha kuthibitisha uwezo wake wa kuyakata mayenu.

Hata hivyo, umati uliohudhuria tamasha hilo, ulinong’ona kwamba Lulu ni mcharuko kwa sababu alipoitwa jukwaani, alitakiwa kucheza sebene kidogo lakini yeye alinengua kuliko wanenguaji wa Twanga.

Paparazi wetu alikuwepo uwanjani hapo na kumshuhudia Lulu akicheza mpaka ‘kugalagala’ sakafuni kama picha ukurasa wa kwanza zinavyozungumza.

Pamoja na kumponda kwa kuonesha ‘ucharuko’ wake, kundi lingine lilimfagilia kuwa siku akishindwa uigizaji, anaweza kulamba mshahara wa nguvu kwenye bendi kubwa Bongo kutokana na uwezo wake wa kunengua.

“Anajua kucheza, yaani siamini kama ni Lulu. Kumbe siyo kwenye filamu tu, hata kwenye muziki ni mkali,” Vicky Mushi mkazi wa Soweto alizungumza baada ya kushikwa na hamasa.

Mbali na Lulu, mastaa Vincent Kigosi ‘Ray’, Steven Kanumba, Isa Musa ‘Cloud’, Jacob Steven ‘JB’ na wengineo walicheza sebene lakini hawakufua dafu kwa mauno ya ‘bi mdogo’.

Ukiachana na tukio hilo, Bongo Movie Club waliacha gumzo Moshi ambapo tamasha hilo, lilikusanya umati mkubwa wa watu.


HABARI PICHA Na Imelda Mtema, GLobal Publishers Tz

No comments:

Post a Comment