Saturday, August 6, 2011


NA GLADNESS MALLYA (GPL)
Shugamami Wema Isaac Sepetu (pichani) anajuta kuwa na ushosti na waigizaji Jacqueline Steven Pentzel ‘Jack wa Chuz’ na Rose Donatus Ndauka akidai kuwa eti, kwa sasa wanampotezea.

Akihojiwa na kituo kimoja cha redio jijini Dar juzi kuhusu kuvunjika kwa kundi lao la JAROWE ambalo lilikuwa limekamilisha filamu moja iliyokwenda kwa jina la The Diary, Wema alisema amekuwa akitaka kujua juu ya kazi yao hiyo lakini kila akiwatafuta Jack na Rose, amekuwa akikata tamaa kufaidi matunda ya kazi yao hiyo.

“Nikimpigia simu Jack ananiuliza wewe nani wakati anajua namba na sauti yangu. Kusema kweli najuta kuwafahamu Jack na Rose na nahisi wanataka kunipiga changa la macho,” alisema Wema.

Risasi Jumamosi lilimtafuta Rose lakini hakupatikana na alipopatikana Jack wa Chuz ili kupata undani wa kile Wema anacholalamikia kuwa yeye na Rose wameamua kumpotezea na kuhisi kwamba wanataka kumpiga changa la macho, alifunguka: “Sitaki kusikia jina la Wema masikioni mwangu, naomba mniulize ishu nyingine lakini isiwe inamhusu Wema kwa sababu tumemchoka.”

No comments:

Post a Comment