Tuesday, July 5, 2011

Shibuda asema atawaeleza wananchi kuhusu maovu ya Mbowe na Zitto na ubinafsi CHADEMA


Mbunge wa Maswa Magharibi, John Shibuda, amesema hatishiki na vitisho vinavyofanywa na viongozi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) na yuko tayari kufukuzwa katika chama kwa kosa la kusema ukweli siku zote.

Katika maelezo yake, Shibuda, ambaye alihamia CHADEMA mwaka jana akitokea CCM, baada ya kushindwa katika kura za maoni, alisema pamoja na kwamba Mbowe na Zitto wanaamini wako sahihi, ukweli utabaki pale pale kwamba wanasiasa hao wanahatarisha demokrasia katika chama hicho.Hivi karibuni, Shibuda amedaiwa kwenda kinyume cha msimamo wa chama chake, kuhusiana na suala la posho za wabunge, kitendo ambacho kimemfanya aonekane muasi ndani ya chama na hivyo kuundiwa tume ya kumchunguza.

No comments:

Post a Comment