Saturday, July 30, 2011

MKUTANO MAALUMU WA UTAFITI MUONGOZO NA TIBA YA KUONDOA WIZI WA KAZI ZA WASANII WA FILAMU NA MUZIKI TANZANIA.

MOBILES 0715 316 796, 0717 729 577.

P O BOX 4779 DAR ES SALAAM.

NDUGU WAHARIRI

VYOMBO VYA HABARI,

YAH; MKUTANO MAALUMU WA UTAFITI MUONGOZO NA TIBA

YA KUONDOA WIZI WA KAZI ZA WASANII WA FILAMU

NA MUZIKI TANZANIA.

Ndugu Wahariri wa vyombo vya habari,

Awali napenda kuwashukuru nyie binafsi na taasisi zenu kwa ujumla na kutambua mchango wenu katika maendeleo yaliyoanza kujitokeza katika tasnia ya filamu nchini.

Pamoja na hayo bado tasnia yetu ina changamoto nyingi za kufikia maendeleo halisi, changamoto hizo baadhi ni uhaba wa elimu miongoni mwa wadau wa tasnia, tatizo la soko la uhakika kwa kazi zetu, tatizo la maharamia wa kazi zetu (piracy),tatizo la maadili miongoni mwetu n.k.

Shirikisho la Filamu Tanzania TAFF,limeanzishwa kwa lengo la kutafuta njia na namna ya ufumbuzi wa mataizo hayo kwa kutumia rasilimali mbalimbali za ndani ya tasnia na nje pia ili kufikia malengo.

Kutokana na hayo kampuni ya Fred Promotion iliamua kufanya utafiti wa jinsi ya kupata njia sahihi ya kuondoa “Piracy” na namna kuwa na mfumo wa usambazaji utaoleta tija.

Baada ya kukamilika kwa rasimu ya tafiti, tafiti hiyo ilikabidhiwa kwa Viongozi wa TAFF na kuupitia,baada ya kuipitia vyema, Uongozi wa TAFF imeamua wadau wa tasnia nao wakausikia ili kuongeza tafakuri pana zaidi kwa maendeleo ya tasnia.

Ndugu Wahariri kwa kutambua nafasi yenu na weledi mlio nao katika maendeleo ya tasnia hii tunawaalikakuhudhuria mkutano huo utaofanyika 29.07.2011 Kuanzia saa 4:00 asubuhi mpaka saa 7:00 mchana, katika ukumbi wa Baraza Sanaa la Taifa(BASATA) Ilala mjini Dar es Salaam.

Mwisho ni matarajio yetu utakuwa pamoja nasi,nakutakia kazi njema.

WILSON R. MAKUBI

KATIBU MTENDAJI

No comments:

Post a Comment