Friday, July 8, 2011

DINGI AMLAWITI MWANAE WA MIEZI 6


Baba mmoja mwenye akili timamu aliyefahamika kwa jina la Leny Love (29), amekamatwa kwa kosa la kumlawiti mtoto wake wa kiume wa miezi sita na kumuambukiza Ukimwi.

Kwa mujibu wa polisi, baba huyo kutoka mji wa Silverton, Ohio, wakati akifanya unyama Machi mwaka huu alikuwa akijua kuwa ni muathirika wa virusi vya Ukimwi.

Leny alikamatwa Ijumaa iliyopita na kufunguliwa mashitaka ya ubakaji, kosa la kumiliki bangi na shambulio. Polisi wamesema walipomhoji baba huyo alikiri makosa.

Kwa sasa anashikiliwa katika Kituo cha Sheria cha Kati cha Hamilton County wakati akisubiri kesi yake kufikishwa mahakamani.

Baadhi ya watu waliosoma habari hiyo mtandaoni walionesha kusikitishwa na kitendo hicho huku wengine wakisema siyo bure.

“Huu ni unyama na hii siyo bure. Mwanao wa kumzaa tena mdogo kiasi hicho unamlawiti huku akikuangalia? Jamani tunakwenda wapi? Mungu atuepushie matukio haya kwenye jamii yetu,” alisema mama Josin wakati akitoa maoni yake mtandaoni juu ya habari hiyo.

No comments:

Post a Comment