Friday, July 22, 2011

BARNABA & SHILOLE....Baaaaaasi!


Na Gladness Mallya, Global Publishers
MSANII wa filamu Bongo, Zuwena Mohamed ‘Shilole’ amemtapika aliyekuwa
mpenzi wake Elias Barnaba kwa madai kuwa hivi karibuni amemdhalilisha.

Akizungumza na Ijumaa juzi Shilole alisema kuwa, uhusiano wa kimapenzi kati yake na Barnaba haukuwa na kificho ila kwa kuwa ameonesha kutokuwa na msimamo,
bora waachane tu.

“Hakuna asiyejua kuwa Barnaba ni mpenzi wangu na yeye mwenyewe alikuwa anajitangaza na gari yangu alikuwa anaitumia na siku alipoondoka nilimsindikiza lakini nashangaa huku nyuma ameacha maneno mengi kuwa hawezi kutembea na mimi kwa sababu eti mimi ni mkubwa, nimeolewa na nina mtoto,” alisema Shilole.

Aliendelea kudai kuwa, Barnaba ni mwanaume aliyezidiwa na tamaa na yeye ndiye aliyemchoka kwa hiyo anamsubiri akirudi kutoka Marekani, wanaachana rasmi.

Katika siku za hivi karibuni Shilole na Barnaba wamekuwa wakidaiwa kuwa ni wapenzi lakini juzikati Barnaba aliruka kimanga na kudai kwamba hawezi kutoka na msanii huyo wa filamu kwani ni shugamami kwake.

No comments:

Post a Comment