Saturday, June 25, 2011

Tamko la Serikali kuhusu bei ya dawa mseto ya malaria

Katibu Mkuu Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, Blandina Nyoni amesema dawa ya mseto ya Malaria hairuhusiwi kuuzwa zaidi ya Shilingi 1,000/= (elfu moja tu) kwa dozi ya mtu mzima na Shilingi 500/= (mia tano tu) kwa dozi ya mtoto.

Tamko hilo la Serikali linafuatia kuwepo kwa taarifa na vitendo vya uuzwaji wa dawa mseto ya Malaria yenye alama ya kijani ambayo ina punguzo maalum, kuuzwa kwa bei ya juu katika baadhj ya maduka ya dawa na vituo vya afya nchini Tanzania.

Nyoni amesema punguzo hilo ni moja ya jitihada za Serikali za kukabiliana na tatizo hilo la Malaria ambao ni ugonjwa unaoathiri watu wengi katika nchi za Bara la Afrika ikiwemo Tanzania.

source: http://www.wavuti.com/4/post/2011/06/tamko-la-serikali-kuhusu-bei-ya-dawa-mseto-ya-malaria.html#ixzz1QGvgciKi

No comments:

Post a Comment