Friday, June 3, 2011

TAMASHA LA KUMI LA KIMATAIFA LA SERENGETI FIESTA 2011


Kufanyika kwa Tamasha la Kumi la Kimataifa la Serengeti Fiesta 2011 nchini kutatoa mchango mkubwa katika ukuzaji wa uchumi wa mwananchi mmoja mmoja na taifa kwa ujumla kutokana na shughuli mbalimbali za kibiashara zitakazofanyika ndani ya msimu wa fiesta mwaka huu.

Mwenyekiti wa kamati ya Maandalizi ya Tamasha la Serengeti Fiesta 2011, RUGE MUTAHABA amesema tamasha hilo litawakusanya takribani watu elfu ishirini kwa wakati mmoja ambapo matarajio yake Watanzania wataendelea kunufaika kiuchumi kama ilivyokuwa miaka iliyopita.
Kuhusiana na Msanii wa Kimataifa atakayekuja kutoa burudani kwUzinduzi rasmi wa tamasha hilo unatarajiwa kufanyika kesho ambapo ratiba ya matukio mbalimbali yatakayofanyika kwenye msimu wa Serengeti Fiesta mwaka huu itatangazwa kwenye tamasha hilo MUTAHABA anasema.

No comments:

Post a Comment