
GHARAMA ya kumuona mkali wa miondoko ya dancehall, Orville Richard Burrell maarufu kama Shaggy, atakapokuwa visiwa vya Zanzibar kufunga rasmi tamasha la filamu la kimataifa la nchi za jahazi (ZIFF) itakuwa ni Sh 5000 kwa wananchi na wageni kutoka ughaibuni itakuwa ni dola 10.
Katika onesho hilo litakaloanza saa tatu usiku viti maalumu vitakuwa Sh 30,000. Shaggy atatumbuiza katika Uwanja wa Amaan, Zanzibar Jumamosi usiku wa Juni 24 baada ya kukamilika kwa utoaji wa tuzo kwa filamu bora zilizoingia katika mashindano.
Na Beda Msimbe
No comments:
Post a Comment