Friday, June 17, 2011


National Arts Council BASATA

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
MWALIKO WA WASANII KUSHIRIKI MAONYESHO NA MAUZO YA 16 YA KIMATAIFA MJINI RHO ITALIA TAREHE 3-11/12/2011
Baraza la Sanaa la Taifa kupitia wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo.limepokea taarifa ya wasanii wa Tanzania kutakiwa kushiriki Maonyesho ya 16 ya sanaa ya Kimataifa yatakayofanyika Mjini Rho, Italia.

Maonyesho haya yanalenga bidhaa za asili na za kiutamaduni kutoka nchi mbalimbali duniani zikiwemo za Asili (typical products) , Muziki (Musical events), Ngoma (Dances), Mapambo (colours) na vyakula (flavours) ambazo kwa ujumla wake zinaelezea historia ya nchi na watu wake.

Baraza linahimiza vyama na mashirikisho ya sanaa, wasanii, wadau wa sanaa kutumia fursa hii kuonyesha kazi mbalimbali za sanaa katika Tamasha hilo hapo
juu.

Kwa maelezo zaidi juu ya maonyesho haya, wasanii na wadau wa sanaa watembelee tovuti ya www.artigianoinfiera.it au kuwasiliana na waandaaji kupitia barua pepe cratfsfair@gestionefiere.com au kwa simu +39 02 31911911 au nukushi +39 02 31911920.

Ghonche Materego
KATIBU MTENDAJI

No comments:

Post a Comment