Monday, June 27, 2011

MWANAMUZIKI SHAGGY ATAWAZWA KUWA CHIFU NA BALOZI WA KABILA LA WASUKUMA BUJORA, MWANZA

Chifu Charles Kaphipa akizungumza katika tamasha hilo la Bulabo kabla ya kumtawaza mwanamuziki Shaggy, wanaosikiliza kutoka kulia ni Chifu Makwaiya, Meneja wa kinywaji cha Serengeti Lager Allan Chonjo Allan Chonjo, Mkurugenzi wa Masoko wa SBL Caroline Ndungu, Mwanamuziki Shaggy na Mzee Mark Bomani.

Mwanamuziki Shaggy akishangilia huku akiwa amepunga usinga na kupewa sapoti na vigoli wa kabila la kisukuma mara baada ya kutawazwa kuwa chifu wa kabila la wasukuma, katika tamasha la ngoma za asili la Siku ya Mavuno yaani (Bulabo) kwa Kisukuma lililofanyika katika kijiji cha Kisesa mahali ambapo pana makumbusho ya Bujora yaliyohifadhi tamaduni zote za kabila la wasukuma.

Mwanamuziki Shaggy wa Marekani akiondoka kwa kucheza huku akiwa ameshikilia usinga na kusindikizwa na vigoli wa kabila la kisukuma wakati alipokuwa akiondoka katika eneo la tukio mara baada ya kutawazwa kuwa chifu wa kabila la wasukuma, katika tamasha la ngoma za asili la Siku ya Mavuno yaani (Bulabo) kwa Kisukuma lililofanyika katika kijiji cha Kisesa mahali ambapo pana makumbusho ya Bujora yaliyohifadhi tamaduni zote za kabila la wasukuma.

No comments:

Post a Comment