Saturday, June 11, 2011

Mchungaji adai kutaja wauza madawa kumsaidia Rais Kikwete

“Si kwamba tutataja majina ya maaskofu na wachungaji pekee, bali tutataja hadi wale waliomo ndani ya Ofisi ya Rais, ambao wanafanya biashara hiyo, wabunge pamoja na mawaziri,” alidai mchungaji wa Kanisa la Evangelical Pentecost Church (TEC) la mjini Mbeya, William Mwamalanga.

Moto wa kauli hii ulichochewa na maelezo ya ofisi ya rais kuwaonya maaskofu wa jumuiya ya kikristo Tanzania ambao walitoa saa 48 kwa rais kuyataja majina ya hao wahusika
wa kuuza madawa a.k.a unga.

Mwishoni mwa wiki iliyopita wakati Rais Kikwete akihutubia waumini wa Kanisa Katoliki la Mtakatifu Killian katika sherehe ya kuwekwa wakfu na kusimikwa Mhashamu Askofu John Ndimbo, kuwa askofu wa Jimbo la Mbinga, alikaririwa akisema baadhi ya viongozi wa dini wamekuwa wakishiriki kufanya biashara ya dawa za kulevya.

Ikulu iliweka bayana kuwa viongozi wa dini si malaika au watakatifu hapa duniani, kwani wanaweza kutumbukia katika majaribu na kujikuta katika vitendo au hali isiyo tegemewa katika jamii.

No comments:

Post a Comment