Thursday, June 23, 2011

MAMA WEMA AIFUMUA JAROWE


Kwa mujibu wa chanzo cha habari, mama mzazi wa Wema, Mariam Sepetu ndiye mchokonoaji baada ya kudai kuwa, ‘memba’ mmoja wa kundi hilo, Jack wa Chuz anamharibu binti yake huyo.

Inadaiwa kuwa, mama huyo na familia nzima imekuwa ikimtuhumu Jack wa Chuz kuwa ndiye anayemfanya Wema ashindwe kutulia nyumbani na matokeo yake anafanya mambo ya ajabu.

Chanzo kiliendelea kuweka kweupe kuwa, lawama hizo zilitokea nje ya Kituo cha Polisi Kijitonyama ‘Mabatini’ jijini Dar es Salaam ambapo mama Wema alisikika akimlalamikia Jack kwamba, ndiye kiini hasa cha mwanaye kuharibika tabia.

Aidha, chanzo kingine kikasema kuwa, mama huyo alidai tangu mwanaye arudi kutoka Marekani alifikia kwa Jack na hasikii la mtu yeyote.

“Mama Wema alikuja juu, akadai mwanaye alifikia kwa Jack alipotoka Marekani, amekuwa hasikii la mtu yeyote yule,” kilisema chanzo.

CHANZO: Global Publishers Tz

No comments:

Post a Comment