Njemba mmoja mkazi wa Mbagala Sabasaba Wilaya ya Temeke jijini Dar es Salaam, Seleman Mohamed (48) anashikiliwa na Jeshi la Polisi, Kituo cha Chang’ombe baada ya kufiwa na hawara yake wakiwa kitandani.
Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake mwishoni mwa wiki iliyopita, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kipolisi Temeke, ACP David Misime alisema wanamshikilia Mohamed kufuatia kifo cha hawara yake aliyemtaja kwa jina la Elizabeth Costance (40) aliyefariki Mei 31, mwaka huu wakiwa wamelala kitandani nyumbani kwake Mbagala Sabasaba.
Kamanda Misime alisema kuwa Mohamed alipotoka katika matembezi yake alifika nyumbani kwake akiwa na mwanamke huyo anayedaiwa kuwa ni mpenzi wake Mei 30, mwaka huu ambapo walilala pamoja na ilipofika kesho yake saa 12.30 asubuhi Elizabeth alikata roho.
No comments:
Post a Comment