Friday, June 24, 2011

HAKI YA NANI....MISS TZ 2011 YUKO MORO!

WASHIRIKI WA SHINDANO LA MISS MOROGORO 2011 KWENYE PICHA YA PAMOJA NA WAKUFUNZI WAO, MRATIBU, MKURUGENZI WA FG ARTS PROMOTION, NA WAWAKILISHI WA WADHAMI WAO. AMBAO NI REDDS NA VODACOM TANZANIA.

WASHIRIKI WA SHINDANO LA MISS MOROGORO 2011 KWENYE PICHA YA PAMOJA WAKIPATIWA ELIMU YA MAZINGIRA KUFUATIA KAULI MBIU YA SHINDANO HILO MWAKA HUU, AMBAYO NI “BETTER ENVIROMENT TODAY” (BET).

WASHIRIKI WA SHINDANO LA MISS MOROGORO 2011 KWENYE PICHA YA PAMOJA WAKIPATIWA ELIMU YA MAZINGIRA KUFUATIA KAULI MBIU YA SHINDANO HILO MWAKA HUU, AMBAYO NI “BETTER ENVIROMENT TODAY” (BET).

BAADHI YA WASHIRIKI WA SHINDANO LA MISS MOROGORO 2011 WAKIPATA KIFUNGUA KINYWA KAMBINI MWAO KWENYE HOTELI YA MASUKA VILLAGE MOROGORO.

MREMBO JACKLYN KITINKA AKIWA NA WASHIRIKI WENZIWE KWENYE CHAKULA CHA JIONI KAMBINI MWAO KWENYE HOTELI YA MASUKA VILLAGE MOROGORO.


Lile shindano kubwa la ulimbwende Tanzania linaendelea kushika kasi hasa katika ngazi ya mikoa, ambapo FG ARTS PROMOTION AND ENTERTAINMENT wameahidi kumtoa mrembo wa Tanzania 2011 kutokea MJI KASORO BAHARI - MOROGORO.

Akitanabaisha kwa undani zaidi Soul Makini, amesema warembo wa Morogoro mwaka huu wamejipanga ipasavyo kuweza kutoa Miss Tz 2011. Warembo wapatao 15 watashea jukwaa moja ndani ya Morogoro Hotel kuwania taji la mwakilishi wa morogoro 'MISS MOROGORO 2011' mnamo tarehe 1/7/2011.

Shindano hilo litanogeshwa na burudani kabambe kutoka kwa wakali wa Manzese - TIP TOP Connection sambamba na mkali wa ngoma za asili Wanne Star. Kiingilio kitakuwa 10,000/ kwa mtu mmoja.

No comments:

Post a Comment